Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatrajia kutoa hatifungani yake ya kwanza ya Sukuk wakati wowote kuanzia tarehe 22 Februari 2025. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni maalumu iliyoundwa na serikali (Zanzibar Treasury Sukuk1 Limited) kwa ajili ya kutoa hattifungani hiyo, Waziri wa Nnchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt Saada Mkuya Salim alisema. "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kutoa hatifungani ya Sukuk kwa ajili ya kuwezesha miradi ya maendeleo ya Serikali na kuwapa fursa Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kidini, walioko ndani na nje ya Tanzania, kuwekeza katika hatifungani hii". Hatifungani hii ya serikali inayozingatia misingi ya Shari'ah (Halal) itakuwa ya kwanza katika eneo lote la Afrika Mashariki na Kati. Ni aina ya Ijara Sukuk na itakuwa na faida (siyo riba) ya asilimia 10.5 kwa mwaka itkayolipwa kwa awamu mbili na ni ya miaka saba (7). Awali akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Zanzibar Treasury Sukuk1 Limited, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, CPA Juma Amour, aliipongeza serikali ya Zanzibar kwa kutekeleza ndoto ya muda mrefu kuhusu Sukuk. Mchakati wa Sukuk hii unaoongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Yusra Sukuk Company Limited, Sheikh Mohamed Issa, taasisi ambayo ndiyo Mshauri Elekezi aliyepewa kazi hiyo na Serikali ya Zanzibar. Tukio la Uzinduzi wa Sukuk ya Zanzibar linatarajiwa kufanyika tarehe 22 Februari 2025 katika viwanja vya Ikulu Zanzibar na kuongozwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kuhudhuriwa na wageni mbali waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi za nje na washirika wa maendeleo. Hii ni fursa adhimu kwa Watanzania kuwekeza fedha zao kw anjia ya Halal. Bodi ya Ushauri wa Kishari'ah chini ya Kituo cha Usimamizi wa Masual aya Kifedh ana Udhubiti (CIFCA) inaongozwa na Prof. Hamed Hikmany, ilikabidhi cheti cha Sukuk ya Zanzibar kukidhi masharti ya Shari'ah (yaani Shari'ah Compliant Certificate) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya SPV, CPA Juma Amour mbele ya Waziri Saada Mkuya, wanahabari na waalikwa wengi. Katika hatifungani hii ya Sukuk ya Zanzibar, kuna washauri elekezi wengine saba (7) ambao ni CIFCA, Lawfields Advocates and Legal Consultants, BM Attorneys, BDO-Tanzania, PBZ Ikhlas, CSDR, Sovereign Africa Ratings (ya Afrika ya Kusini) na ZIC Takaful.
This an event article, used for writing about and listing the events planned for the future on your website. You can edit all of this text from the Pages tab by clicking the edit button.
This an event article, used for writing about and listing the events planned for the future on your website. You can edit all of this text from the Pages tab by clicking the edit button.
This an event article, used for writing about and listing the events planned for the future on your website. You can edit all of this text from the Pages tab by clicking the edit button.